Dalili za filamu iliyowatokea jana Barcelona zilianza kuonekana kama zinawatokea Real Madrid, hadi dakika ya 90 Juventus tayari walikuwa mbeleni kwa mabao 3 kwa 0 katika dimba la Santiago Bernabeu.
Shukrani kwa muamuzi Michael Oliver ambaye dakika ya 92 alitoa tuta kwa Real Madrid ambalo liliwapa bao ambalo liliitupa nje ya michuano ya Ulaya Juventus huku mlinda lango wao Gianluigi Buffon akipewa kadi nyekundu.

Huko Allianz Arena Bayern Munich walisuluhu bao sifuri kwa sifuri na Sevilla, matokeo haya yanawafanya Barca kufudhu kwa aggregate ya bao 2-1 baada ya ushindi walioupata Hispania wiki iliyopita.

Post a Comment